BEMBA to be transferred to ICC.
2 Julai 2008BRUSSELS.
Mahakama ya Ubelgiji imeondoa vipingamizi vyote ili kuwezesha aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini J.K ya Kongo, Jean Pierre Bemba kupelekwa mjini the Hague kujibu mashtaka ya uhalifu wa kivita. Mahakama kuu ya Ubelgiji imepinga madai yaliyotolewa na mawakili wa Bemba kwamba taratibu za kisheria zilizofuatia ,baada ya kukamatwa kwake mjini Brussels mnamo mwezi mei hazikuwa sahihi.
Hatua ya kumpeleka Bemba kwenye mahakama ya kimataifa inayopambana na uhalifu ,ICC mjini the Hague ilikuwa inasubiri uamuzi wa mahakama.
Uamuzi huo unatarajiwa kutekelezwa karibuni.
Bemba alikamatwa katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels mwezi mei kufuatia hati ya kisheria ya mahakama ya kimataifa ya ICC. Anakabiliwa na mashtaka manne ya uhalifu wa kivita na mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu anayodaiwa kutenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.