1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki kuu duniani zapunguza riba wakati ukosefu wa ajira ukiongezeka

Mohamed Dahman5 Desemba 2008

Benki Kuu duniani kote zimezidisha harakati za kupambana na hali ya kuporomoka kwa uchumi na matatizo ya mikopo hapo jana kwa hatua kubwa za kupunguza viwango vya riba wakati watu wakiendelea maradufu kupoteza ajira zao.

https://p.dw.com/p/G9sb
Rais wa Benki Kuu ya Ulaya Jean-Claude Trichet.Picha: AP

Hata hivyo hatua hiyo ya kupunguza riba za benki imeshindwa kuinuwa masoko ya hisa.

Benki Kuu ya Ulaya imepunguza kiwango chake kikuu cha riba kwa kuvunja rekodi kutoka asilimia 0.75 hadi kuwa asilimia 2.50 wakati mkuu wa benki hiyo Jean-Claude Trichet akionya kwamba uchumi wa kanda ya nchi zenye kutumia sarafu ya euro unaweza kuanguka kwa hadi asilimia 1.0 hapo mwakani.

Amesema kwa kuzingatia tathmini ya hivi sasa wanaona uchumi dhaifu duniani na kuzorota sana kwa mahitaji ya ndani ya nchi kukiendelea katika kipindi cha muda fulani unaokuja.

Benki Kuu ya Uingereza nayo imepunguza kiwango chake kikuu cha raiba kwa asilimia 2.0 na kulingana na kile cha chini kabisa cha wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia huo ukiwa ni ushahidi unaongezeka kwamba nchi hiyo inakabiliwa na uporomokaji mkubwa wa kiuchumi.

Tawkimu za Umoja wa Ulaya zimethibitisha makadirio ya awali kwamba kanda ya Ulaya inayotumia sarafu ya euro ya mataifa 15 iko katika ushukaji wake wa kwanza wa uchumi ukipunguwa kwa asilimia 0.2 katika vipindi viwili vilivyopita vya robo mwaka.

Akizungumzia hali hiyo ambayo imeathiri vibaya sekta kuu ya magari duniani Rais wa Shirikisho la makampuni ya magari la Ujerumani Matthias Wiisman amesema mgogoro huu haukuathiri tu nchi moja au kanda moja kama ilivyokuwa hapo zamani safari huu umeathiri masoko yote muhimu duniani.

Wakuu wa makampuni makubwa kabisa ya magari nchini Marekani wa General Motors na Chrysler LLC wamesema watafikiria kuanza upya mazungumzo ya kuziunganisha kampuni hizo iwapo itabidi ili kuweza kupatiwa fungu la hadi dola bilioni 34 katika msada wa dharura wa serikali ya Marekani.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Genreal Mototrs Rick Wagoner ameiambia kamati ya benki ya baraza la senate nchini Marekani hapo jana kwamba atakuwa tayari kuliangalia suala hilo kwa makini.

Pia ameahidi kuzingatia utengenezaji wa magari yenye ufanisi wa matumizi ya mafuta na kupunguza gharama za uzalishaji.

Ingawa kuna maseneta walioelezea kutouamini uongozi wa makampuni hayo ya magari wabunge wengi wa Marekani wamesema hawawezi kuachilia sekta hiyo isambaratike.

Hakuna hatua yoyote ya msaada inayoweza kuchukuliwa kabla ya wiki ijayo na pengine hata zaidi licha ya tahadhari kubwa zilizotolewa kwamba kampuni ya General Motors inaweza kusambaratika kufikia mwishoni mwa mwezi wa Desemba bila ya kupatiwa msaada.

Wakati sokol la hisa la Wall Street mjini New York Marekank likifunguliwa kwa biashara wawekazaji wametambuwa kwamba kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu ya AT na T imetangaza kwamba inapunguza ajira za watu 12,000 pamoja na kupunguza matumizi ya mtaji kutokana na kuporomoka kwa uchumi.

Upunguzaji wa ajira pia umetangazwa na kampuni kubwa ya habari Vaicom na kampunmi ya kutengeneza madawa ya DuPont

Repoti ya serikali inaonyesha kupunguwa kwa madai mapya ya watu wanaopoteza ajira katika kipindi cha wiki moja iliopita lakini kiwango cha watu waliopoteza ajira zao kinaendelea kuwa kikubwa cha watu 509,000.