1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Bayern Munich mabingwa wa kombe la Ujerumani.

29 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF99

Mabingwa wa ligi ya soka nchini Ujerumani Bayern Munich wamekamilisha ushindi wa mara ya tano wa kunyakua vikombe viwili katika msimu mmoja, nchini Ujerumani jana Jumamosi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Schalke 04 katika mpambano wa fainali katika kombe la Ujerumani .

Bayern imeshinda ubingwa wa ligi kwa kupata points 77 kutokana na michezo 34 ya ligi, ambapo makamu bingwa ni Schalke ambao wamemaliza kampeni ya msimu huu kwa kujikingia points 63.