1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kansela kukutana na rais wa Korea ya kusini mjini Berlin leo.

13 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNi

Rais wa Korea ya kusini Roh Moo Hyun atakutana na kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder mjini Berlin leo.

Hatua ya Korea ya kaskazini ya kutengeneza silaha za kinuklia ni suala litakalochukua nafasi ya mbele kabisa katika mazungumzo hayo.

Bwana Roh alikutana na viongozi wa shughuli za viwanda na biashara jana katika kujadili nafasi ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara na Ujerumani.