1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ludger Vollmer waziri mdogo wa zamani wa mambo ya nje wa ujerumani ajitetea kuhusu sakata ya kashfa ya visa

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKk

Naibu wa waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani Ludger Vollmer,amekanusha madai dhidi yake yaliyotolewa na upinzani kwamba alirahisisha kuingia ujerumani wahalifu na wahamiaji haramu kutoka Ulaya mashariki.

Akitoa ushahidi wake mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kile kinachojulikana kama kashfa ya Visa,Volmer alisema aliiagiza sheria za utoaji visa katika ubalozi wa Ujerumani kwa watu wa Ulaya mashariki zilegezwe kwa ajili ya sababu za kibinadamu. Mwanasiasa huyo wa chama cha kijani alisema mabadiliko hayo yalilenga kurahisisha familia kutembeleana kiurahisi.

Alijitetea kwa kuongeza kusema kuwa hatua hiyo ilikuwa imeungwa mkono na wabunge kutoka pande zote za upinzani wakati ilipotangazwa miaka mitano iliyopita. Jumatatu ijayo ni zamu ya waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Ficher kutoa ushahidi wake mbele ya kamati hiyo.