BERLIN: Majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yamalizika
19 Januari 2007Matangazo
Maafisa wa Marekani na Korea ya Kaskazini wamekamilisha majadiliano ya siku tatu katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin.Majadiliano hayo yamehusika na mradi wa kinuklia wa Korea ya Kaskazini.Ingawa mpatanishi mkuu wa Marekani Christopher Hill hapo awali alisema mazungumzo hayo yalikuwa ya maana,hakueleza zaidi alipoondoka Berlin kuelekea Asia.Lakini alidokeza kuwa ni matumaini yake kuwa mazungumzo ya kundi la pande sita huenda yakafanywa hivi karibuni.