1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Mfumo wa afya wafanyiwa mageuzi.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5z

Serikali ya muungano mkuu nchini Ujerumani imefikia makubaliano juu ya mpango wa mageuzi ya mfumo wa afya nchini humo.

Makubaliano hayo yanafikisha mwisho wiki kadha za malumbano baina ya chama cha kansela Angela Merkel cha Christian Democrats na kile cha Social Democrats na yanaonekana kuwa muhimu kwa ajili ya uhai wa serikali yake.

Kansela Merkel ametangaza hatua hiyo baada ya zaidi ya saa saba za majadiliano kati ya washiriki wa serikali hiyo ya mseto.

Mageuzi hayo yana lengo la kuweka gharama za afya kwa wafanyakazi kutozidi na kuimarisha ukuaji wa uchumi. Sehemu kuu katika mageuzi hayo yataanza kutekelezwa mwaka 2009, mwaka mmoja kuliko ilivyopangwa hapo kabla.