BERLIN: Rais wa Korea Kaskazini akaribishwa Ujerumani.
11 Aprili 2005Matangazo
Rais wa Korea Kaskazini Roh Moo Hyun amepokelewa rasmi na rais wa shirikisho la Ujerumani Horst Köhler katika ziara yake ya siku tano nchini Ujerumani.
Mbali na masuala ya kiuchumi mada nyingine muhimu watakazozingumzia viongozi hao ni pamoja na maswala yanayohusu Korea kaskazini na Iraq.
Vile vile mazungumzo hayo yatahudhuriwa na kansela Gerhard Schröeder.
Rais Roh Moo Hyun anapendelea pia kujifunza kutokana na maarifa na mafanikio ya muungano wa Ujerumani mbili.