BERLIN: Steinmeier asema Korea Kaskazini na Iran ni tishio la amani duniani
18 Oktoba 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier amelieleza jaribo la kinyuklia la Korea Kaskazini na mzozo wa nyuklia wa Iran, kuwa vitisho vikubwa kwa usalama wa dunia.
Aidha Steinmeier amesema migogoro yote miwili inauhatarisha mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha za kinyuklia kwa sababu huenda izishawishi nchi jirani zitake pia kujihami na silaha za kinyuklia.
Katika mahojiano yake na jarida la Stern la hapa Ujerumani, waziri Steinmeier ameihimiza Korea Kaskazini irudi katika meza ya mazungumzo na mataifa sita akisema hajui mtu yeyote anayetaka kuutanzua mzozo wa Korea Kaskazini kutumia harakati za kijeshi.