BERLIN.Bunge lapitisha mageuzi katika sekta ya afya
2 Februari 2007Matangazo
Bunge la Ujerumani limepitisha mpango wa mageuzi katika sekta ya afya baada ya mvutano wa muda mrefu.
Watetezi wa mpango huo wamesema kuwa lengo la mageuzi hayo ni kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.
Chini ya mpango huo serikali itaunda shirika kubwa la bima litakalokusanya fedha na kuzigawa miongoni mwa mashirika ya bima ya umma yanayowahudumia wananchi wengi.
Kansela wa Ujerumani akiwa ni mtetezi wa mageuzi hayo amesema.
Otton……….
Lengo la mabadiliko hayo ni kutoa huduma bora zaidi na kuwapa wananchi uwanja mkubwa wa kuchagua. Aidha yataimarisha ushindani na kuhakikisha ugharamiaji.
Wapinzani wa mabadiliko hayo wanahoji kuwa pana nakisi kubwa baina ya mapato na matumizi.