1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mawakala wa CIA kukamatwa

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCWD

Mahakama moja hapa Ujerumani inaagiza kukamatwa kwa watu 13 waliohusika na njama ya utekaji nyara inayodaiwa kuungwa mkono na Shirika la Ujasusi la marekani la CIA.Njama hiyo ilimhusisha raia mmoja wa Ujerumani anayedhaniwa na Marekani kuwa mshukiwa hatari wa ugaidi.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka walioko mjini Munich kusini mwa Ujerumani hati za kukamatwa kwa watu hao wanaodhaniwa kuwa wakala wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA zimeshaidhinishwa.Watu hao wanakamatwa kwa kushukiwa kuteka na kusababisha madhara ya mwili katika njama hiyo.

Serikali inafanya uchunguzi kuhusu madai kuwa Khaled el Masri raia wa Ujerumani aliye na asili ya Lebanon alitekwa na mawakala wa Marekani katika mji mkuu wa Macedonia wa Skopye katika mkesha wa mwaka mpya,mwaka 2003.

Kqwa mujibu wa Masri aliye na umri wa miaka 43 na muuzaji magari wa zamani,yeye alikamatwa na kusafirishwa hadi nchini Afghanistan kuhojiwa kabla kuachiwa huru miezi baada ya mitano nchini Albania.Bwana Masri anadai kuwa aliteswa alipokuwa kizuizuini.