Berlin.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani anatazamiwa kuwasili DRC baadae hii leo.
26 Septemba 2006Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung akiwa katika ziara ya siku tatu ya kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani katika nchi za kiafrika, amewasili Libreville nchini Garbon.
Amewatembelea wanajeshi 430 waliowekwa katika mji mkuu huwo wa Garbon tayari kuwasaidia wenziwao waliopo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akiwa Djibout katika pembe ya Afrika Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung alisema hafikirii kama muda wa operesheni za jeshi la wanamaji wa Ujerumani katika pembe ya Afrika zitamalizika haraka.
Waziri wa ulinzi amesema.
“Ningependelea zaidi kuona ushirikiano pamoja na nchi zinazopakana na eneo hilo, ili kuweza kuziandama meli hata katika maeneo yao ya bahari na hivyo kurahisisha ukaguzi katika maeneo hayo. Hili ninavyoamini mimi ni moja wapo ya mada zinazohitaji kuimarishwa”.
Baadae hii leo waziri wa ulinzi anatazamiwa kwenda Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amepangiwa kuzungumza na mwenyekiti wa kamisheni huru ya uchaguzi Apollinaire Malumalu pamoja na watetezi wawili wa kiti cha urais Joseph Kabila na Jean-Pierre Bemba.
Ujerumani imetuma wanajeshi 740 kusaidiana na wanajeshi 2,500 wa nchi za Ulaya ili kusimamia usalama katika uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.