Bernard Membe, Tanzania
23 Mei 2013Matangazo
"Katika kipindi cha miaka 50, mataifa yote 54 ya Kiafrika sio tu yamejishughulisha na ukombozi wa kisiasa bali pia wa kiuchumi. Changamoto katika kipindi hicho cha miaka 50 zilikuwa nyingi na tofauti. Kwa mfano kurejea desturi mbaya za kunyakuwa madaraka kupitia mapinduzi. Halafu,vita vya wenyewe kwa wenyewe: Tuna matatizo makubwa nchini Somalia na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tunaona lakini pia kuna juhudi za kimataifa kuipatia ufumbuzi mizozo hiyo. Miaka 50 ya Umoja wa Afrika inatukumbusha Tanzania na mchango mkubwa wa nchi yetu na serikali yetu chini ya uongozi ya muasisi na baba wa taifa letu, marehemu Mwalimu Julius Nyerere."