Biden atoa msamaha wa rais kwa mwanawe Hunter
2 Desemba 2024Hunter Biden mwenye umri wa miaka 54, alikiri makosa hayo na natarajiwa kuhukumiwa wiki chache zijazo kabla rais mteule wa Marekani Donald Trump kuchukua hatamu za uongozi.
Hatua hii inamaliza gumzo la muda mrefu kuhusiana na mwanawe Biden, ambaye mwezi mmoja baada ya babake kushinda uchaguzi wa mwaka 2020, alifichua hadharani kwamba alikuwa anachunguzwa na Mahakama.
Biden wakati huo aliapa kuheshimu utawala wa sheria lakini kutokana na hatua hiyo, Rais huyo wa Marekani anayemaliza muda wake madarakani amekwenda kinyume na ahadi yake ya awali ya kutotumia nguvu zake za urais kwa manufaa ya familia yake.
Mnamo Novemba 8 baada ya ushindi wa Trump, msemaji wa ikulu ya White House Karine Jean-Pierre aliondoa uwezekano wa msamaha kwa Hunter akisema, "tumeulizwa swali hili mara kadhaa. Jawabu letu bado ni lile lile, hapana."
Rais mteule Donald Trump ametaja msamaha wa Biden kwa mwanaye kuwa hujuma kwa haki.