Biden azuru mradi wa reli nchini Angola, anapomalizia ziara
4 Desemba 2024Matangazo
Marekani na washirika wake wamewekeza katika ukarabati wa mradi huo mkubwa wa reli wa kilomita 1,300 unaoziunganisha Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Angola. Serikali yaBidenimesema mradi huo wa reli utasaidia kuimarisha maslahi ya kibiashara lakini pia kukabiliana na ushawishi wa China unaoimarika barani Afrika.Mradi huo unalenga kuendeleza ushawishi wa Marekani katika eneo hilo lenye utajiri wa madini ya kobalti, shaba na mengine muhimu yanayotumika kutengeneza betri, magari ya umeme na vifaa vya kielektroniki.