Serikali ya Tanzania ipo katika hatua ya kutaka kupitisha sheria itakayowafanya watu wote kuwa katika mfuko wa bima ya Afya. Lengo ni kuondoa changamato zinazowakabili wananchi wengi na hasa wa vijijini. Katika kipindi cha Kinagaubaga Grace Kabogo amezungumza na Bernard Konga ambae ni mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF.