Bin Laden ataka Ulaya iondowe wanajeshi wake Afghanistan
30 Novemba 2007Matangazo
Kiongozi wa Al Qaeda Osama bin Laden amezitaka nchi za Ulaya kuondowa wanajeshi wao kutoka Afghanistan.
Kwenye ukanda mpya wa video uliorushwa hewani na kituo cha televisheni cha Kiarabu cha Al Jazeera hapo jana bin Laden amewataka wananchi wa Ulaya kuzishinikiza serikali zao kujitowa Afghanistan.
Bin Laden kwa mara nyengine amekubali kuwajibika na mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani lakini amesema kundi la Taliban wakati huo likiwa madarakani nchini Afghanistan lilikuwa halijuwi kitu juu ya mipango ya mashambulizi hayo.
Wakati huo huo wanajeshi wawili wa Danmark wameuwawa hapo jana wakati wakipambana na waasi wa Taliban katika jimbo la Helmand kusini mwa Afghanistan.