Video hii itakupeleka moja kwa moja hadi ndani ya jengo moja la kawaida katika mji wa Marburg lililo kaskazini magharibi mwa Ujerumani, ambako utaona mfanyakazi wa kampuni ya dawa ya BioNtech anavyotengeneza chanjo aina ya mRNA, inayotumika kuwakinga watu dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Ni kazi inayohitaji umakini mkubwa!