Blinken: Wakaazi wa Gaza wanakabiliwa na uhaba wa chakula
19 Machi 2024Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema watu wote wa Gaza wanakabiliwa na "viwango vikubwa vya uhaba wa chakula," huku akisisitiza umuhimu wa kuzidisha kasi katika uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu katika ardhi ya Palestina. Aidha Blinken amesema.
Soma taarifa hii: Blinken azungumza na Israel juu ya pendekezo la Hamas
Blinken ameeleza kuwa "madhumuni ya safari ya Misri na Saudi Arabia ni mengi. Bila shaka, ni kushinikiza makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka. Kama unavyojua, tunashughulikia mno suala hilo kila siku na tunafanya kila tuliwezalo ili kuendeleza mpango huu na kufikia makubaliano. Lakini pia ni kuendeleza mazungumzo ambayo tulianza mnamo Januari kuhusu hatma ya Gaza baada ya vita na hatua ambazo zitahitaji kuchukuliwa ili kuhakikisha utawala, usalama na usaidizi wa kibinadamu, kwa ajili ya kuijenga upya."
Ripoti ya UN: UN: Nusu ya wakaazi wa Gaza wanakabiliwa na baa la njaa
Hayo yakiarifiwa mapigano makali yameendelea kuripotiwa katika ukanda wa Gaza ambapo wizara ya afya eneo hilo inayodhibitiwa na Hamas imesema watu 20 wameuawa hii leo kufuatia mashambulizi ya Israel.