1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOMBAY: India kuanzisha tena huduma za reli na Pakistan

24 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEP5

India imesema huenda ikaanzisha tena huduma za usafiri wa reli na Pakistan mwezi Januari mwakani. Njia hiyo kati ya mji wa Kokhrapar nchini India na mji wa Munabao nchini Pakistan ilifungwa wakati wa vita ya pili vya dunia. Kwa sababu ya uhusiano mbaya kati ya mataifa hayo mawili, reli hiyo haikufunguliwa.

Katika miaka michache iliyopita maofisa wa huduma za usafiri wa reli kutoka mataifa hayo wamekuwa wakikutana kujadili kuanzisha tena huduma hizo. Njia ya kwanza ya reli kati ya Lahore na Amritsar, India ilifunguliwa mwezi Januari mwaka huu.