1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOMBAY:Uchunguzi waendelea nchini India juu ya mashambulio ya mabomu

12 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8C

Polisi ya India inafanya uchunguzi wa kutafuta wahusika wa mashambulio ya mabomu yaliyofanywa kwenye mtandao wa Treni katika mji wa kibishara wa Mumbai ambapo watu 190 wameuwawa na zaidi ya 625 wakajeruhiwa.

Polisi wamefanya msako katika mji huo wa Mumbai kuwatafuta magaidi waliotekeleza mashambulio hayo,

Hadi sasa hakuna mtu aliyedai kuhusika na mashambulio hayo ambayo serikali ya India inasema yalipangwa kwa ustadi mkubwa.

Wanamgambo wa Kashmir wanaoshukiwa na serikali ya India kwamba huenda walihusika wamekanusha kuhusika na vilevile wameyalaani mashambulio hayo.