1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA-Burundi kuwatimua wafyanakazi wa Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada wanaowasaidia Wanyarwanda wanaokimbia mashtaka ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

25 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAV

Serikali ya Burundi imetishia kuwatimua wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kimataifa,watakaopatikana kuwasaidia kwa siri,raia wa Rwanda ambao wameyakimbia makazi yao,kuepuka kutiwa hatiani kutokana na kushiriki kwao katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Rais wa Burundi Domitien Ndayizeye amesema ataamuru wafanyakazi hao kutimuliwa,kama ripoti zitathibitisha kuwa vikundi hivyo vya kutoa misaada vinawaondoa Wanyarwanda kutoka eneo la mpakani na kuwaweka katika kambi ndani ya Burundi,akisema hii ni kukiuka makubaliano kati ya serikali ya Kigali na ya Bujumbura.

Akiwahutubia maofisa wa jeshi,Rais Ndayizeye amevitaja vikundi vinavyotiliwa mashaka ni pamoja na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi-UNHCR.

Hata hivyo mashirika hayo mawili ya kimataifa hayajasema lolote kuhusiana na madai ya Rais huyo wa Burundi.