1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA Chama cha FDD chashinda uchaguzi nchini Burundi

6 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEx0

Chama cha kundi la waasi wa zamani wa kabila la Hutu nchini Burundi FDD, kimeshinda uchaguzi wa bunge uliofanyika nchini humo. Maofisa wa uchaguzi wamesema chama hicho kiliongoza kwa idadi kubwa ya kura. Chama tawala cha wahutu kinachoongozwa na rais Domitien Ndayizeye kilichukua nafasi ya pili, huku chama kikuu cha watutsi kikifuata katika nafasi ya tatu.

Uchaguzi huo ni utangulizi wa kumchagua rais mpya wa taifa katika mpango wa amani unaolenga kumaliza miaka 12 ya umwagikaji damu nchini humo. Wabunge 100 wanaounda bunge la Burundi, wajumbe wa seneti watakaochaguliwa mwezi huu wa Julai na wanachama wa mabaraza ya kijamii, watamchagua rais mpya mwezi Agosti.