1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA : Makamo wa Rais Burundi ajiuzulu

5 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDF7

Alice Nzomukunda ambaye ni afisa mwandamizi nambari mbili katika serikali ya chama tawala nchini Burundi amewaambia waandishi wa habari mjini humo kwamba asingeliweza kuendelea kupuuza matukio ya usumbufu nchini humo nchi ambayo imekuwa katika mtihani wa amani baada ya miaka 12 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Nzomukunda amesema uamuzi wake umechochewa na matatizo kadhaa ya kisiasa ambayo wanakabilina nayo wananchi wa Burundi ikiwa ni matatizo ya usalama,kutoheshimiwa kwa sheria, usimamizi mbaya wa fedha za taifa na wa sheria ya haki za binaadamu ambazo zinakiukwa.