1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura. Makundi ya waasi wa zamani wa Kihutu nchini Burundi waelekea kupata ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6s

Kundi la zamani la waasi wa Kihutu nchini Burundi limeonesha kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini humo, ukiwa ni uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi katika muda wa miaka 12.

Burundi imefanya uchaguzi huo muhimu kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa watakaoongoza wilaya 129 siku ya Ijumaa , kabla ya kufanya uchaguzi wa bunge na rais wenye lengo la kuimarisha demokrasia baada ya machafuko ya kikabila yaliyochukua muda wa zaidi miaka kumi.

Uchaguzi huo unaonekana kuwa kipimo cha nguvu kati ya vyama 30 vya Wahutu na Watutsi ambavyo vinagombania viti katika mabaraza ya serikali za mitaa katika nchi hiyo iliyogawika kati ya makabila ya Watutsi na Wahutu ambao ni asilimia 85 ya jumla ya watu wote nchini humo wanaofikia milioni nane.