1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA. Mapigano yalipuka Burundi

10 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF51

Mapigano yamelipuka kati ya vikosi vya jeshi la Burundi na wanamgambo wa FNL katika maeneo ya mji mkuu wa Bujumbura Mpanda na Kabumba watu zaidi ya sita wameuwawa.

Kundi la waasi nchini Burundi FNL limeilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kukiuka mapatano ya kusimamisha mapigano ya mwezi Mei 15 baina ya rais Domitiyen Ndayizeye na kiongozi wa waasi Agathon Rwasa, katika juhudi za kumaliza vita katika taifa hilo lililokubwa na vita kwa muongo mmoja.

Lakini serikali ya Burundi imekanusha madai hayo ya kundi la Forces for Nationa Liberation FNL.

Pasteur Habimana msemaji wa wawakilishi watano wa kundi hilo la waasi la FNL ametoa malalamiko hayo mjini Dar es Salaam Tanzania ambako leo mazungumzo ya utaratibu wa kusalimisha silaha yamepangiwa kuanza mjini humo.

Kwa upande wake msemaji wa serikali ya Burundi Pancreas Cimpaye amesema kuwa bila ya kuwepo wasimamizi wa kimataifa mtu yeyote anaweza kutumia silaha kiholela na baadae kuilaumu serikali kwa makosa hayo.

Serikali ya Burundi haikusema lolote kuhusu nani hasa´aliye anzisha mapigano mapya yaliyozuka nchini humo jumanne iliyopita lakini imelilaumu kundi la FNL kwa shambulizi la kombora la kurushwa kwa mkono katika kiunga kimoja mjini Bujumbura.

Kuanzishwa tena kwa mazungumzo baina ya serikali ya Burundi na waasi wa FNL kunaleta matumaini ya kupatikana kwa amani nchini Burundi.