1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA : Polisi 4 wahukumiwa kifo kwa mauaji ya mwakilishi wa WHO

4 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFH0

Mahkama ya Burundi hapo jana imewahukumu kifo maafisa wanne waandamizi wa polisi kwa kuhusika na mauaji ya mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO nchini humo hapo mwaka 2001.

Kassi Manlan aliuwawa na mwili wake kutupwa kwenye kingo za Mto Tanganyika.

Maafisa hao wamehukumiwa kifo bila ya wao kuwepo mahkamani wakati maafisa wengine tisa wamehukumiwa vifungo kati ya miaka 2 gerezani hadi vifungo vya maisha.

Mahkama ya Rufaa nchini Burundi imewaona polisi hao wanne Emile Manisha,Gerard Ntunzwenayo, Japhet Ndayegamiye na Aloys Biziman kuwa na hatia ya kupanga mauaji ya Manlan juu ya kwamba wamekataa kukiri kuwa na hatia.