1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA: Sheria ya kuunda halmashauri ya kuwapokonya wanaomiliki silaha nchini Burundi yasainiwa

6 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFG1

Rais wa Burundi Domitien Ndayizeye ametia saini sheria ya kuunda Halmashauri yenye jukumu la kuwapokonya silaha wale wote wanaozimiliki kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa sheria hiyo raia wa Burundi wameamriwa kusalimisha silaha zao la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria .

Sheria hiyo mpya inaimarisha sheria iliyopitishwa mwaka 1971 ambayo adhabu ya watakaomiliki silaha kinyume cha sheria watafungwa au watanyongwa.

Lakini tume ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi imesema kuwa zoezi hilo lisitumiwe kama hoja ya kuhairishwa kwa mara nyingine tena uchaguzi wa Burundi.