1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA. Shughuli za uchaguzi Burundi.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNW

Shughuli za uchaguzi nchini Burundi zimepiga hatua baada ya bunge la senate nchini Burundi kuipitisha miswaada miwili ya uchaguzi na kijamii.

Rais wa senate Libere Bararunyeretse aliwaeleza waandishi wa habari kuwa miswaada hiyo miwili sasa itawasilishwa bungeni na kwamba tume ya uchaguzi nchini Burundi itawajibika kubadili ratiba ya uchaguzi hadi miswaada hiyo itakapopitishwa rasmi na bunge.

Uchaguzi nchini Burundi ulipangiwa kufanyika mwezi huu wa nne.