1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA : Tanzania kuwatimuwa waasi wa Burundi

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7I4

Balozi wa Tanzania nchini Burundi ameonya hapo jana kwamba nchi yake itawatimuwa viongozi waandamizi wa kundi la waasi la Burundi iwapo halitomaliza mazungumzo ya amani kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Balozi Francis Bernard Mdolwa amekaririwa akisema kwamba watakuwa hawawatimui waasi hao bali watakuwa wanajifukuza wenyewe.

Viongozi wengi wa kundi la waasi la mwisho lililobakia nchini Burundi wanaishi nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na msemaji wao na kamanda mmoja mwandamizi.

Waasi hao na serikali ya Burundi wametia saini makubaliano ya kusitisha mapigano hapo mwezi wa Septemba mwaka jana lakini juhudi za kutekeleza makubaliano hayo zimeshindwa kufanikiwa hadi sasa.