1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA :Tanzania yakutana na waasi wa FNL wa Burundi

29 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFSZ

Maafisa waandamizi wa serikali ya Tanzania na viongozi kutoka kundi pekee la waasi lililobakia nchini Burundi wameanza mazungumzo mjini Dar es Salaam hapo jana kwa lengo la kuanzisha mazungumzo rasmi ya amani na serikali ya Bujumbura.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Therence Sinunguruza amethibitisha kwamba majadiliano na kundi la waasi la FNL yanaendelea hivi sasa mjini Dar es Salaam lakini serikali ya Burundi haihusiki.

Mwanadiplomasia mmoja mjini Bujumbura amesema kuanza kwa mazungumzo hayo hapo jana ambayo yamemjumuihsa Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania ni hatua nzuri ambayo yumkini ikafunguwa njia ya kufanyika kwa mazungumzo rasmi ya amani na kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu nchini Burundi.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo aliyekataa kutajwa jina lake amesema mazungumzo hayo yamefikia ngazi mpya na yanaonekana kama maandalizi ya mazungumzo kati ya serikali ya Burundi na waasi wa FNL.