1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura. Uchaguzi nchini Burundi wakamilika, matokeo kupatikana baadaye leo

5 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CExD

.

Uchaguzi wa bunge umemalizika nchini Burundi. Uchaguzi wa hapo jana ni hatua ya hivi karibuni katika mpango unaoungwa mkono na umoja wa mataifa wenye nia ya kumaliza miaka 12 ya machafuko ya kikabila nchini humo.

Msemaji wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi amewaambia waandishi wa habari kuwa zoezi la kuhesabu kura limeanza na kwamba matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kuanzia baadaye leo.

Chama cha Wahutu cha FDD, Movement for the Defence of Democracy kinapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Vyama 25 vimeshiriki katika uchaguzi huo.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi kati ya Wahutu ambao ndio wengi na Watutsi ambao ni wachache na ambao wanahodhi madaraka makubwa kisiasa nchini humo vimeua watu zaidi ya 300,000.