1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA: Wakatoliki wa Burundi waomboleza kifo cha muwakilishi wa Vatikan nchini Burundi

30 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFnl

Muwakilishi wa makao matakatifu ya Vatican nchini Uganda, Askofu Pierre Christophe, amewasili katika mji mkuu wa Burundi - Bujumbura leo asubuhi, siku moja baada ya kuuwawa na watu wenye silaha katika eneo la kusini mwa mji wa Bujumbura, aliekuwa muwakilishi wa Vatican nchini Burundi, Askofu Michael Courtney. Muwakilishi wa Vatican nchini Uganda, amewaambia waandishi wa habari punde baada ya kuwasili mjini Bujumbura, kwamba ametumwa na Papa John Paul wa pili, kwenda Burundi kujiunga na wakristo wa nchi hiyo, katika msiba uliowafikia. Alipoulizwa kuhusu wapi na lini yatafanyika mazishi ya marehemu, alisema bado hajajadiliana na wakuu wa kanisa katoliki nchini Burundi, kuhusu maada hiyo. Katibu mkuu wa Jumuia ya Umoja wa Mataifa Dr. Koffi Annan amelaani mauwaji dhidi ya aliekuwa muwakilishi wa Vatican nchini Burundi, Askofu Michael Courtney. Koffi Annan amesema Jumuia ya Umoja wa mataifa, imemkosa mtu mwenye busara ambae alitoa mchango mkubwa katika juhudi za kutafuta amani ya Burundi.