BUJUMBURA: Wananchi wameshiriki katika kura ya maoni ya kihistoria nchini Burundi..
1 Machi 2005Matangazo
Wananchi wa Burundi wameshiriki katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia katika miaka kumi na mbili iliyopita.
Zaidi ya watu milioni tatu walijiandikisha kushiriki katika kupiga kura ya maoni ambayo itaamua katiba ya nchi hiyo na kuitayarisha Burundi kwa uchaguzi mkuu utakao leta usawa wa uongozi kwa makabila ya Burundi.
Iwapo katiba hiyo itakubalika basi taifa hilo litaweza kuunda mfumo wa kugawana mamlaka baina ya Wahutu walio wengi na Watusi wachache walioshikilia madaraka ya kisiasa na kijeshi tangu taifa la Burundi lilipo jipatia uhuru wake mwaka 1962.
Zaidi ya watu laki tatu wameuwawa kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1993 nchini Burundi vilivyozuka baada ya kuuwawa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo.