BUJUMBURA:Wanajeshi wauwa watu wanne Burundi
10 Novemba 2003Matangazo
Vikosi vya wanajeshi wa Burundi vimewapiga risasi na kuwauwa watu wanne na kujeruhi wengine saba wakati wakiwasaka waasi wa Kihutu karibu na mji mkuu wa Bujumbura hapo jana.
Mauaji hayo yalitokea wakati vikosi hivyo vilipokuwa vikiwatafuta wapiganaji wa Kihutu wenye misimamo mikali wa kundi la FNL kwa kukizingira kijiji cha Muyira kilioko katika mkoa wa Bujumbura vijijini kilomita 11 kaskazini mwa Bujumbura muda mfupi baada ya kuingia alfajiri.
Kwa mujibu wa mashahidi wa tukio hilo idadi kubwa ya vijana walikamatwa kwa ajili ya kuhojiwa na wanajeshi walifyetuwa risasi wakati vijana kadhaa walipojaribu kukimbia. Jeshi la Burundi halikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tukio hilo.