1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA:Waruanda waliotorokea Burundi kurejeshwa kwao

13 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF42

Serikali ya Rwanda na Burundi zilizokutana hapo jumamosi zimewataja wanyaruanda waliotorokea nchini Burundi kuwa wahamiaji haramu.

Baadhi ya wakimbizi elfu 8 wakinyaruanda wapo katika makao ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa.

Duru za serikali ya Burundi zinasema Zoezi la kuwarudisha kwa nguvu wakimbizi hao litaanza hapo kesho siku ya jummanne.

Kanali Dicace Nzikoruriho,ambaye anahusika na wakimbizi katika wizara ya mambo ya ndani ya Burundi,amesema wakimbizi wa Rwanda lazima warejee kwao akiongeza kusema kuwa hali hivi sasa inatishia aman katika eneo hilo.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wakimbizi,UNHCR; limeitaka serikali ya Burundi kuughairi uamuzi wake na badala yake iangalie suala la kutoa hifadhi kwa wakimbizi hao.

Wengi wa Wakimbizi hao wakiwa wahutu walikimbilia nchini Burundi kutokana na hofu ya ya kukabiliwa na mashtaka ya kuhusika kwenye mauji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.