1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BURUNDI : Rais mpya kuifanya Burundi mfano wa Afrika

27 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhN

Rais mpya wa Burundi Piere Nkuruzinza hapo jana ameapishwa kuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia baada ya vita vya miaka 12 na kuahidi kuifanya nchi hiyo kuwa mfano wa Afrika kwa kuijenga kwa kuzingatia msingi wa mafanikio yake ya kukomesha miaka ya 12 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyouwa watu 300,000.

Kiongozi huyo ameapa kupiga marufuku itikadi zote zile zenye kugawa watu kwa misingi ya kikabila na kusababisha mauaji ya halaiki pamoja na kupiga vita rushwa ambalo ni tatizo kuu kwa nchi nyingi za Kiafrika.

Nkurunzinza mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni kiongozi wa zamani wa waasi wa Kihutu amechaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano chini ya katiba ya kushirikiana madaraka ilioidhinishwa hapo mwezi wa Februari.