1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi: Wanafunzi wa bweni sharti wapime COVID-19

Amida ISSA,12 Aprili 2021

Wanafunzi wote wa bweni nchini Burundi walazimika kupima virusi vya COVID-19 ndipo waruhusiwe kuingia shuleni kuendelea na masomo ya muhula wa tatu. Lengo ni kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3rtPf
Burundi Covid-19-Tests
Picha: DW/A. Niragira

Muhula wa tatu na wa mwisho wa masomo ya mwaka 2020/2021 umeanza nchini Burundi. Kulingana na maagizo yaliotolewa na rais wa nchi hiyo Evariste Ndayishimie, hakuna mwanafunzi anaruhiwa kuingia shuleni pasipo kupima Covid-19, katika hatua ilionuwiwa kusaidia kudhibiti ugonjwa huo.

Philothe Hakizimana, mkurugenzi wa shule ya sekondari ya Skeppes ilioko kata ya Nyakabiga mjini Bujumbura, amesema hakuna mwanafunzi aliyeruhusiwa kuingia shuleni Jumatatu pasi na kuonesha kuwa tayari amefanyiwa kipimo cha Covid 19.

Soma pia: Hali ya COVID-19 ikoje mpakani mwa Burundi na Tanzania?

Zoezi hilo la kuwapima wanafunzi kirusi cha Covid 19 linaendeshwa na manesi kutoka wizara ya afya ambapo tangu jumapili hii wamekuwa wakiwapima wanafunzi wanao rejea katika shule mbali mbali baada ya likizo ya pasaka.

Mkurugenzi Philothe Hakizimana ameongenza kusema kuwa wanafunzi ambao tayari wamefanyiwa vipimo wanawekwa sehemu mmoja na kutengwanishwa na wale ambao bado wanasubiri kufanyiwa kipimo cha Corona.

Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi
Rais Evariste Ndayishimiye wa BurundiPicha: Getty Images/AFP/T. Nitanga

Kwenye shule ya upili ya Vugizo zoezi hilo pia limefanyika. Mkurugenzi wa shule hiyo Alphonse Niyonzima amesema kwenye shughuli za masomo hazikufanyika kwani wamekuwa katika heka heka za kuhakikisha wanafunzi wanafanyiwa kipimo cha Covid 19.

"Hapa kwenye shule ya Lycee Vugizo zowezi la kuwapima wanafunzi linafanyika tangu jana. Wale ambao tayari wamepimwa ikiwa wale wanao ishi katika mabweni na wanaotokea nyumbani tumewaweka pamoja tukisubiri wanafunzi wote wafanyiwe vipimo ili shughuli za masomo ziweze kuanza," amesema Niyonzima.

Hadi majira ya mchana wa Jumatatu, wanafunzi 60 pekee kwenye shule ya upili ya Skeppes Nyakabiga ndiyo walikuwa tayari wamerudi shuleni na kupimwa Covid 19, kati ya jumla ya 420 wanao soma katika shule hilo.

Uamuzi wa kuwapima wanafunzi umetajwa na serikali ya Burundi kama mojawapo ya hatua ya kupambana na kuenea kwa virusi vya corona.
Uamuzi wa kuwapima wanafunzi umetajwa na serikali ya Burundi kama mojawapo ya hatua ya kupambana na kuenea kwa virusi vya corona.Picha: Marco Passaro/Independent Photo Agency Int./imago images

Mkurugenzi Philothe Hakizimana amesema kuna umuhimu timu ya manesi wanaowafanyia wanafunzi kipimo cha Corona kusalia hapo kwa muda wa siku 4 hadi wiki.

"Hawa wanafunzi wanao ishi katika mabweni wengi wanatoka mikoa ya mbali mbali. Hadi leo wamekwisha wasili 60 peke, shule ikiwa na wanafunzi 450. Baadhi ya wanafunzi hutatizwa na uwezo kifedha wa kulipa karo za shule, na wengine kwenye siku kama hizi usafiri inakuwa shida, tungeitaka wizara ya afya timu hii kusalia ikiendesha vipimo kwa muda wa siku 4 hadi wiki moja," amesema Philophe.

Baadhi ya wakurugenzi wa shule waliotaka wahifahiwe majina yao wamesema wapo baadhi ya wanafunzi ambao baada ya kufanyiwa vipimo wamekutwa wakiwa na kirusi cha Covid 19.

Wizara ya afya na kupambana na janga la ukimwi ilisitisha zoezi la kutanganza kila baada ya wiki 2, idadi ya raia waloambukizwa COVID-19 na hali jumla ya maambukizi ya janga hilo inavyoendelea nchini.

Zoezi hilo la kuwapima wanafunzi limefanyika kufuatia amri ya Rais Evariste Ndayishimiye aliyebaini kuwa kuna umuhimu hata wanafunzi kujuwa hali yao ya afya kufuatia janga la covid 19.