1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi yawaachia huru wafungwa 4,000 kupunguza msongamano

27 Novemba 2024

Takriban wafungwa 4,000 wameachiliwa huru na serikali ya Burundi kama sehemu ya kampeni inayolenga kupunguza msongamano katika jela za taifa hilo la Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/4nUbb
Burundi Gefängnis Feuer Brand Gitega
Vikosi vya usalama na maafisa wengine wamekusanyika nje ya gereza la Gitega, Burundi Jumanne, Des. 7, 2021.Picha: ASSOCIATED PRESS/AP/picture alliance

Rais Evariste Ndayishimiyealitangaza msamaha kwa wafungwa wengi mapema mwezi huu, akisema utawahusu tu wafungwa waliotuhumiwa kwa makosa madogo ya uhalifu na akautetea uamuzi huo kuwa hatua ya kupunguza gharama. Kiasi ya wafungwa 5,500 kwa jumla wanatarajiwa kuachiwa huru kutoka megerezani, ambayo yanawahifadhi wafungwa zaidi ya mara tatu ya uwezo wao. Taarifa ya ofisi ya rais imesema kuwa kiasi ya wafungwa 4,000 kati ya 5,442 waliopewa msamaha tayari wamesharejea kwa familia zao. Lakini kiongozi wa shirika la haki za binaadamu nchini humo, Iteka, Anschaire Nikoyagize amekashifu ukweli kwamba wafungwa wa kisiasa, ambao idadi yao ni kati ya 4,000 na 5,000, hawakujumuishwa kwenye msamaha huo wa rais.