Bwawa kubwa la kuzalisha umeme Ethiopia: Mgogoro usiomalizika
Kutoka kwenye ufisadi, matumizi mabaya hadi katika mgogoro wa kidiplomasia: Ujenzi wa bwawa hilo umekumbana na changamoto chungu nzima.
Jengo lililojengwa kwa saruji
Likiwa na urefu wa mita 145, karibu kilometa 2. Bwawa hili linatarajiwa kuwa chanzo kikubwa cha kuzalisha umeme Ethiopia. Kama bwawa kubwa la uzalishaji umeme barani Afrika, litazalisha zaidi ya gigawati 15,000 za umeme kuanzia mwaka 2022. Litatoa maji yake katika mto Nile ambao ni mkubwa barani Afrika.
Muonekano ulivyo kwa sasa
Huku kukiwa na zaidi ya asilimia 50 ya raia wa Ethiopia wanaoishi bila umeme, serikali inataka bwawa hilo kuanza kufanya kazi haraka iwezekanavyo ili mamilioni ya raia wapate umeme.
Bwawa limechukua muda mrefu kujengwa
Ujenzi wa bwawa hili ulianza mwaka 2011, lakini eneo hilo liligunduliwa kati ya mwaka 1956 na 1964. Mapinduzi ya mwaka 1974 yalimaanisha mpango huo haukuweza kusonga mbele hadi mwaka 2009 ambako mpango wa ujenzi ulianzishwa tena. Mradi huu wa dola bilioni 4.6 umekuwa chanzo cha mgogoro wa kimaeneo kufuatia mpango wa kupata maji yake kutoka mto Nile
Kubadilisha Mazingira
Katika miaka michache ijayo eneo hili lote litafinikwa kwa maji. Hifadhi inayohitajika ya kuzalisha umeme inatarajiwa kudhibiti mita za ujazo bilioni 74 za maji. Ethiopia inataka kujaza mto huo kwa maji haraka iwezekanavyo lakini mataifa jirani na taifa hilo yana wasiwasi wa athari ya hatua hii katika mtiririko wa maji yao.
Mkwamo wa Kidiplomasia
Misri, ina wasiwasi kuwa kujaza hifadhi ya maji kwa haraka itahatarisha mtiririko wa maji yake na kuipa nafasi Ethiopia kudhibiti mtiririko wa Mto Nile. Ndio maana Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alikutana na Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi kujadili suala hili.
Bado suluhu haijapatikana
Siku mbili za majadiliano kati ya Ethiopia, Misri na Sudan mjini Washington yalishindwa kutatua suala la hifadhi ya maji licha ya Marekani kuingilia kati kama msuluhishi. Bila ya mafanikio katika miaka minne iliyopita, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alimuita pia rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia mgogoro huu.
Kazi kubwa
Licha ya majadiliano yaliopo wafanyakazi takriban 6000 wapo mbioni kuhakikisha bwawa hili linafanya kazi. Mazingira ya kazi sio ya watu wenye roho ndogo. Katika miezi ya joto kiwango cha joto katika eneo la ujenzi hupanda hadi nyuzi joto 50
Mradi kukumbwa na ufisadi
Katika miaka ya hivi karibuni ujenzi uliahirishwa kufuatia ufisadi unaoendelea na masuala ya usimamizi mbaya wa mradi huo. Mwezi uliopita watu 50 walishitakiwa kwa makosa ya ufisadi unaohusiana na bwawa hilo akiwemo aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme la Ethiopia.