CAIRO:Rais Mubarak atoa wito wa kupuuza uvumi kuhusu afya yake
31 Agosti 2007Matangazo
Rais Hosni Mubarak anatoa wito kwa wanachi wa Misri kupuuza uvumi kuwa afya yake ni mbaya.Kulingana na kiongozi huyo mkongwe aliye na umri wa miaka 79 uvumi huo una misingi ya kisiasa na unalenga kuyumbisha nchi.Kauli hiyo inawagusa zaidi chama kikubwa cha upinzani Muslim Brotherhood kilichopigwa marufuku rasmi japo kupata ushindi wa asilimia 20 ya viti vyote bungeni mwaka 2005.Wawakilishi wa chama hicho waligombea ubunge kama wanasiasa binafsi.
Uvumi huo kuhusu afya ya Rais Mubarak ulianza baada ya yeye kulazwa hospitali,kusafiri ulaya kwa matibabu.
Rais Mubarak ameongoza Misri kwa zaidi ya miaka 25 na kufanyiwa upasuaji mwaka 2004.