CANBERRA: Helikopta ya kutoa misaada yapata ajali
3 Aprili 2005Matangazo
Helikopta ya kijeshi ya Australia imepata ajali katika kisiwa cha Kiindonesia cha Nias.Inakhofiwa kuwa watu 9 waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo wamefariki.Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Australia amesema,helikopta hiyo ilianguka ilipokuwa ikishiriki katika opresheni za misaada inayotolewa katika eneo lililokumbwa na mtetemeko wa ardhi.Kwa upande mwingine wasaidizi kisiwani Nias wamemuokoa mtu aliekuwa chini ya nyumba yake ilioteketezwa na mtetemeko wa ardhi tangu siku tano zilizopita.Wasaidizi bado wanajitahidi kufikisha misaada kwa maelfu ya watu walionasa katika visiwa vya Nias,Simeulue na Banyak. Inakhofiwa kuwa hadi watu 2,000 wamefariki katika eneo hilo.
.