1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN : Rais Putin ziarani Afrika Kusini

5 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFD

Rais Vladimir Putin wa Urusi amewasili nchini Afrika Kusini leo hii kuaza ziara ya kishistoria ya siku mbili ambapo Urusi inatazamiwa kuzidisha uwekezaji nchini humo.

Putin alikaribishwa na waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Nkozana Dalmini Zuma pamoja na maafisa wa Urusi wakati alipowasili kabla ya kuelekea kwenye mazungumzo yake na Rais Thabo Mbeki mjini Cape Town.

Ziara yake ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa taifa wa Urusi kwa eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.