1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League makundi kupangwa leo

29 Agosti 2013

Makundi ya Champions League yanapangwa leo mjini Monaco ambapo timu nne za Ujerumani zinashiriki. Mabingwa Bayern , Dortmund , Leverkusen na Schalke 04 zitajulikana zinacheza katika magundi gani.

https://p.dw.com/p/19YhJ
epa03817833 UEFA General Secretary Gianni Infantino shows a ticket with Kazakstan soccer club Shakhter Karagandy during the draw of the play-offs games of UEFA Champions League 2013/14 at the UEFA Headquarters in Nyon, Switzerland, Friday, August 9, 2013. EPA/LAURENT GILLIERON
Upangaji wa makundi katika Champions LeaguePicha: picture-alliance/dpa

Mshambuliaji maarufu wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo hatahudhuria upangaji leo wa makundi ya kinyang'anyiro cha Champions League mjini Monaco licha ya kuorodheshwa miongoni mwa wachezaji watatu ambao wanatarajia kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika bara la Ulaya.

FC Barcelone' s Argentinian forward Lionel Messi, left, FC Barcelone' s Spanish midfielder Andres Iniesta, center, Real Madrid 's Portuguese forward Cristiano Ronaldo wait the result, during the ceremony of the best player of the year, during the UEFA Champions League draw in Monaco, Thursday, Aug. 30, 2012. (Foto:Claude Paris/AP/dapd)
Messi, Iniesta na RonaldoPicha: AP

Mreno huyo ameorodheshwa pamoja na Lionel Messi wa timu hasimu ya Barcelona na Frank Ribery wa Bayern Munich mabingwa wa sasa wa champions League kuwa wagombea watatu wa tuzo hiyo, lakini badala yake ameamua kusafiri na timu yake ya Real Madrid kwenda katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Deportivo la Coruna.

NYON, SWITZERLAND - APRIL 12: The UEFA Champions League draw balls are prepared for a rehearsal ahead of the UEFA Champions League final draw at the UEFA headquarters on April 12, 2013 in Nyon, Switzerland. (Photo by Harold Cunningham/Getty Images)
Bakuli la kupanga makundiPicha: Getty Images

Ronaldo anasemekana kuwa hakufurahishwa kwa kukiukwa mwaka jana wakati Andres Iniesta wa Barcelona alipotawazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kuingoza Uhispania kufanikiwa kunyakua ubingwa wa mataifa ya Ulaya mwaka 2012.

Leo (29.08.2013)mjini Monaco kutafanyika sherehe hizo za UEFA pamoja na upangaji wa makundi ya timu katika kinyang'anyiro cha Champions League. Timu nne za Ujerumani zitashiriki, ikiwa ni pamoja na mabingwa wa Champions League Bayern Munich, makamu bingwa Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen pamoja na Schalke 04.