1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League yarudi uwanjani leo

3 Machi 2008

Kombe la klabu bingwa larejea uwanjani jumaane kwa Arsenal ikicheza na mabingwa AC Milan.

https://p.dw.com/p/DHL2

Leo (jumaane)ni zamu tena ya duru ya kombe la klabu bingwa barani ulaya-champions League.Arsenal na Manchester United zikiwa zimetengana kwa pointi 1 tu nyu mbani katika premier League zinarudi uwanja ni kujaribu bahati yao –Arsenal ikiwa na miadi na mabingwa wa kombe hili AC Milan ya Itali wakati Manchester inaikaribisha Lyon ya Ufaransa.

Mapambanol mengine hii leo ni kati ya FC Barcelona ya Spain na Celitc –Glasgow ya Scotland.Barcelona lakini iliteleza mwishoni mwa wiki ilipozabwa mabao 4:2 na Atletico Madrid.

Ramadhan Ali anawafungulia pazia la changamoto za jioni ya leo za kombe la klabu bingwa barani ulaya:

Mabingwa watetezi wa kombe hili AC Milan ya Itali wanaikaribisha leo Arsenal mjini Milan wakiimarishwa na na kurejea katika safu yao kwa Kaka-mwanasoka bora wa dunia wa mwaka .Arsenal lakini, ilimudu sare tu ya 0:0 na AC Milan katika Emirates stadium wiki 2 nyuma na katika premier league-ilijionea mwanya wake na Manchester kileleni ukipunguzwa hadi pointi 1.Arsenal itatumai kwahivyo, Emmanuel Adebayor-jogoo lao kutoka Togo lililokosea kidogo tu kuunasa wavu wa Milan wiki 2 nyuma pale mkwaju wake ulipogonga mwamba wa lango la Milan, leo ataiingiza bao.

Carlo Ancelotti ameandaa mtego wsake wa kuinasa Arsenal –mtego ule ule uliozinyima klabu 3 za Uingereza msimu uliopita kombe la Ulaya.

FC Barcelona ilitoka nyuma mara 2 kuizima Celtic na kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 duru iliopita huko Glasgow.Leo wakicheza nyumbani , ndio wanaopigiwa upatu kwamba watacheza duru ijayo licha ya kuzabwa mabao 4-2 mwishoni mwa wiki katika La Liga na Atletico Madrid.

Kocha wa Barcelona, mholanzi Frank Rijkaard alielaumiwa sana kwa kumuacha nje ya chaki ya uwanja muargentina Lionel Messi hapo jumamosi, yamkini sana akamrejesha leo uwanjani kwa changamoto hii na Celtic. Celtic inapasa kuvunja mwiko wake wa kutoshinda nje ya Glasgow katika cha champions league na kushindwa mapambano 15 kati ya 16 iliocheza nje.

Manchester United ilitoka sare bao 1:1 na Lyon huko Ufaransa na bao hilo laweza kuwasaidia leo wakicheza nyumbani kuwapiga kumbo wafaransa uwanjani old Trafford.

Sir Alex ferguson aliwapumzisha jumamosi katika mpambano na Fulham mshambulizi wake Cristiano Ronaldo na Wayne Rooney.Ni wao anaowatazamia leo kuwika mbele ya jogoo la Ufaransa.Pia aliwapimzisha akina Michael Carrick ,Nemanja Vidic na Ryan Giggs.

Lyon ina jukumu la kushambulia ikiwa inataka kufuta bao la Manchester waliokomewa kwao na hii huweza ikawafungulia mlango akina Ronaldo na Wayne Rooney.