Chapisho la Musk kuhusu AfD lawakera wanasiasa wa Ujerumani
21 Desemba 2024Matangazo
Bilionea huyo, alichapisha ujumbe huo kwenye video iliyomuhusu kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha CDU nchini Ujerumani Friedrich Merz.
Serikali ya Ujerumani imejizuia kutoa maoni, lakini wabunge wa pande zote zilizokataa kushirikiana na AfD, walijibu kwa ghadhabu matamshi hayo ya Musk.
Mbunge wa chama cha CDU, Dennis Radtke, alisema inatisha, inakera na haikubaliki kwa mtu muhimu katika serikali ijayo ya Marekani kuingilia kampeni ya uchaguzi wa Ujerumani.
Video hiyo ilimkosoa Merz, anayepewa nafasi kubwa ya kuwa kansela baada ya uchaguzi wa Februari, kufuatia kukataa kushirikiana na chama hicho cha AfD kinachopinga wahamiaji, ambacho kwa sasa kinashikilia nafasi ya pili.