SiasaChina
China yatanua luteka za kijeshi karibu na Taiwan
11 Desemba 2024Matangazo
Hayo yameripotiwa na mamlaka za Taiwan Jumatano, zikisema serikali ya Beijing inataka kuleta matatizo.
Afisa mmoja mwandamazi katika masuala ya usalama wa taifa,ambaye hakutaka kutajwa jina, ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba Luteka kubwa za kijeshi zinazofanywa na Beijing ambazo hazijawahi kuonekana kwa kipindi cha miaka kadhaa zinahusisha kiasi meli 60 za kivita na meli 30 za walinzi wa pwani.
Luteka hizo zinafanyika karibu na visiwa vya Kusini mwa Japan hadi bahari ya Kusini mwa China.
Kadhalika China imeimarisha shughuli za kutumia ndege za kijeshi karibu na kisiwa cha Taiwan katika kipindi cha siku mbili zilizopita.