Christian Lindner atoa wito kwa Wasiyria warudi kwao
25 Desemba 2024Matangazo
Lindner amesema kwa wale waliokuja nchini Ujerumani kutoka Syria kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, kurudi nyumbani inapasa iwe sheria. Hata hivyo waziri huyo wa zamani ameeleza kuwa wale wanaotaka kubakia wanaweza kuomba hifadhi ya kudumu kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji ya Ujerumani.
Lindner amesema kubakia nchini Ujerumani lazima kuambatane na vigezo vinavyoeleweka badala ya kufuata mkumbo. Vigezo hivyo kwa waombaji ni pamoja na kuweza kujikimu kwa kufanya kazi, wawe hawajatenda uhalifu na waitambue katiba huru na ya kidemokrasia ya Ujerumani.