1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CNN-FDD kimejikinghia viti 59 kati ya 100 vya bunge la Burundi

7 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEwd

Kundi la waasi wa zamani nchini Burundi, (FDD) limejipatia viti vingi kabisa kufuatia uchaguzi wa bunge jumatatu iliyopita.Kamisheni kuu ya uchaguzi,CENI ikitangaza matokeo rasmi,imesema chama cha CNDD- FDD kimejinyakulia viti 59 kati ya mia moja vya bunge.Chama cha Frodebu kimejipatia viti 24,Uprona viti 10,CNDD viti vitano na chama cha MRC viti viwili.Matokeo ya mwisho rasmi yanatazamiwa kutangazwa July 20 ijayo.Rais Domitien Ndayizeye amevitolea mwito vyama vyote vya kisiasa viyatambue matokeo hayo ya uchaguzi.Uchaguzi wa bunge unafungua njia ya kuitishwa uchaguzi wa rais agosti 19 ijayo.