Colombia yakanusha kuwepo miili 20,000 uwanja wa ndege
7 Desemba 2024Juzi, Alkhamis, Kamati ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia watu waliopotezwa kwa nguvu ilielezea kwamba "maelfu ya miili isiyotambuliwa ipo kwenye makaburi na maeneo ya kuhifadhia yasiyohudumiwa vyema" ilitaja eneo la uwanja wa ndege wa Bogota.
Hapo jana, meya wa mji huo mkuu wa Colombia, Fernando Galan, alikanusha ripoti hiyo, iliyotolewa baada ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuitembelea Colombia, akiutaka Umoja huo kuthibitisha madai yake.
Soma zaidi: Polisi yagundua miili zaidi na kumtaja mshukiwa wa miili iliyotelekezwa sandukuni
Kitengo maalum cha kuwasaka watu waliotoweka nchini Colombia kinasema watu 104,000 walipotea wakati wa vita kati ya vyombo vya usalama, wapiganaji wa msituni, wanamgambo na makundi ya madawa ya kulevya kuanzia miaka ya 1960.